Batulli ambaye ni mmoja wa waigizaji wa kike warembo nchini na ambaye jina lake halisi ni Yobnesh Yussuph aka Nesh, amefunguka kwenye Twitter kuwa licha ya soko la movie kupanuka, waigizaji wengi hawana kitu.
“Wasanii wengi wa filamu huwa tunaamka asubuhi hata hatujui tutakula nini. Accounts zetu hazina kitu wakati tuna film nyingi sana sokoni,” ametweet.
“Wenzetu huamka na mipango kamili ya siku iliyopo lakini wasanii wa film huwa tunaamka huku tukiwaza ni nani wa kumpiga kibomu siku iende.
"Jina kubwa umejibana umepata gari yako 1 tena used, siku ikiipeleka garage unashinda na wewe huko huko garage kazi zote unasimamisha #Huruma.”
Batulli ameilalamikia pia mikataba mibovu iliyopo kwenye filamu.
“Mikataba ya kazi za film Tanzania ukiisoma unaweza ukajuta kwanini uliamua kuwa muigizaji, unauza movie yako na haki miliki kwa miaka 50.
"Hakuna anaependa ndio maana tunalia na serikali mikataba ibadilishwe tupewe kipaumbele movie niuze leo nimiliki baada ya 50 yrs?
"Unapoenda kuuza kazi halafu tajiri anakupangia bei ya kuinunua pasipo kuangalia gharama ulizotumia ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.”
No comments:
Post a Comment