Sumbawanga. Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani 
Rukwa, imewahukumu watu wanane wa Kijiji cha Sikaungu wilayani 
Sumbawanga, kutumikia kifungo cha miaka 56 jela baada ya kupatikana na 
hatia ya kuteketeza mali za mwekezaji zenye thamani ya zaidi ya Sh 227 
milioni.
                
              
Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Adamu Mwanjokolo, alisema washtakiwa walitenda kosa hilo Oktoba 12 mwaka jana.
                
              
Alisema uhalifu huo waliufanya katika kambi ya 
mwekezaji ambaye ni Efatha Ministry iliyoko Kijiji cha Ulinji ndani ya 
shamba la Dafco Malonje linalomilikiwa na mwekezaji huyo.
                
              
Hakimu Mwanjokolo alisema washtakiwa wamehukumiwa kwenda jela miaka saba kila mmoja.
                
              
Aliwataja watu hao kuwa ni Alexander Kisanko, 
Julius Kazembe, Paul Kazikulima na wenzao watano ambao waliruka dhamana 
wakati kesi ikiwa mahakamani.
                
              
Mwanjokolo alisema ushahidi wa mashahidi sita 
umethibitisha kwamba watuhumiwa kwa pamoja walivamia kambi hiyo na 
kuchoma moto matrekta mawili na magunia 188 ya mahindi.
 
 
No comments:
Post a Comment