Askofu Mkuu wa Kanisa la kiinjili la kiluther Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa (kushoto) akimsimika Mchungaji Dk Fedrick Shoo kuwa Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kaskazini katika ibada iliyofanyika jana katika usharika wa Moshi mjini. Picha na Dionis Nyato
Moshi. Askofu mpya wa Dayosisi ya Kaskazini ya
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo jana
alitoa ujumbe mzito kwa Rais Jakaya Kikwete alipomtaka kuwawajibisha
haraka wahusika kwenye kashfa ya escrow kwa kuwa “viporo vinaumiza
tumbo”.
Dk Shoo aliyemrithi askofu Dk Martin Shao
aliyestaafu, alitoa kauli hiyo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Utawala Bora), George Mkuchika ambaye alimwakilisha Rais, wakati
akihutubia kwenye ibada ya kuwekwa kwake wakfu na kusimikwa kwa msaidizi
wake, Mchungaji Elingaya Saria iliyofanyika Usharika wa Moshi Mjini.
Mbali na Waziri Mkuchika, wengine waliokuwapo
kwenye ibada hiyo ni mawaziri wakuu wa zamani, Frederick Sumaye na
Edward Lowassa, pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyarandu. Pia walikuwapo baadhi ya wabunge na maaskofu wa dayosisi 24.
Katika hotuba yake, Dk Shoo alisema kanisa
linasikitishwa na ufisadi mkubwa unaoendelea miongoni mwa viongozi na
watumishi wa umma na kiburi wanachokionyesha wanapoelezwa ukweli.
“Kinachotusikitisha zaidi ni wahusika kuonyesha
jeuri kubwa na ukakamavu wa hali ya juu pale wanapoambiwa,” alisema Dk
Shoo huku akishangiliwa.
“Mimi sioni mantiki kama mtu amehusika katika mambo fulani, halafu anaanza kusema sikueleweka vizuri halafu anajiuzulu.”
Ingawa hakumtaja kwa jina kiongozi huyo, Jaji
Fredrick Werema alijiuzulu nafasi yake ya Mwanasheria Mkuu kwa
kumwandikia barua Rais akieleza kuwa ushauri wake katika suala la escrow
haukueleweka na umesababisha tafrani.
Katika sakata hilo la Escrow, Jaji Werema ndiye
anayedaiwa kuandika barua akieleza kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti
ya Tegeta Escrow zilipwe IPTL bila ya kukatwa kodi.
“Tunatambua Rais ameanza kuchukua hatua dhidi ya
watu kama hawa. Tunazidi kumwombea yeye na Serikali yetu ili wamwonyeshe
hatua zaidi zinazofaa kuchukuliwa,” alisema Askofu Shoo.
“Panapohitajika kuchukua hatua, tusiweke viporo.
Unajua viporo vikishakuwa vya muda mrefu, vinaumizaa tumbo,” alisisitiza
Dk Shoo huku umati uliofurika ukilipuka kwa furaha na makofi.
Akitangaza uamuzi wake kuhusu maazimio ya Bunge la
Muungano, Rais Kikwete alitangaza kumwondoa kazini Profesa Anna
Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
lakini akasema amemweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhong
No comments:
Post a Comment