Ndege aina ya Cessna 5H-QTT ikiwa imeanguka eneo la Kisongo, karibu na Uwanja wa Ndege Arusha juzi jioni, baada ya kugonga mti wakati ikijiandaa kutua na kusababisha kifo cha mmiliki wake na aliyekuwa rubani, Bob Sambeke
Huu ni msiba wa tatu katika muda wa mwezi mmoja kwani mwishoni mwa mwezi jana, Wakili na Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Nyaga Mawalla alifariki dunia, ikiwa ni siku moja tagu kufariki ghafla kwa mfanyabiashara mwingine wa madini wa mkoani humo,
Arusha/Moshi. Kwa mara nyingine, Mikoa ya
Kilimanjaro na Arusha imetikiswa, kutokana na kifo cha mfanyabiashara
maarufu katika mikoa hiyo, Joseph Sambeke (49) maarufu kama Bob Sambeke.
Bob Sambeke alifariki dunia juzi jioni baada ya
kuanguka na ndege ndogo aliyokuwa akiiendesha, kilomita moja kutoka
Uwanja wa Ndege wa Arusha wakati akitokea mkoani Kilimanjaro.
Huu ni msiba wa tatu katika muda wa mwezi mmoja
kwani mwishoni mwa mwezi jana, Wakili na Mfanyabiashara maarufu mkoani
Arusha, Nyaga Mawalla alifariki dunia, ikiwa ni siku moja tagu kufariki
ghafla kwa mfanyabiashara mwingine wa madini wa mkoani humo, Henry
Nyiti.
Ndege ya Sambeke aina ya MT 7- namba 5H-QTT
ilianguka saa 12.34 jioni baada ya bawa lake kugonga mti katika eneo la
Magereza linalopakana na uwanja huo.
Alijeruhiwa na baadaye alifariki akiwa njiani
wakati akiwahishwa hospitalini na askari wa Magereza ambao wanaishi
katika kambi alipoanguka. Mazishi yake yamepangwa kufanyika Alhamisi
eneo la Karanga, Moshi.
Meneja wa Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede
alithibitisha jana kutokea kwa ajali hiyo, na kueleza kuwa taarifa za
awali zinaonyesha ndege hiyo ni mali ya marehemu Mawalla ambaye alikuwa
mbia wa biashara na Bob Sambeki na imesajiliwa kupitia Kampuni ya
Quality Tours & Travellers.
Hata hivyo, Wakili Alex Msando, ambaye pia alikuwa
mshirika wa Mawalla, aliliambia gazeti hili kuwa Sambeke alikuwa
ameinunua ndege hiyo kutoka kwa marehemu.
Dede alisema ndege hiyo, ilianguka mita 200 kutoka
njia namba 8 ya kuruka ndege katika uwanja huo ikitokea Kilimanjaro,
katika dakika 15 za muda wa nyongeza wa matumizi ya uwanja huo.
Alisema ndege hiyo ikiongozwa na rubani Bob
Sambeki ina uwezo wa kubeba watu wanne akiwamo rubani. Baadhi ya
walioshuhudia tukio hilo, walisema kabla ya kuanguka ndege hiyo, ilikuwa
ikiyumba na iligonga mti mkubwa katika moja ya mabawa yake na kupoteza
mwelekeo.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Julias Laizer
alisema kwamba aliona ndege hiyo ikigonga mti na kuyumba, kisha
kudondoka chini na ndipo askari wa magereza walipojitokeza kutoa msaada.
Laizer alisema Sambeki alikuwa peke yake na alijeruhiwa kichwani.
Kifo chake
Taarifa za kifo chake zilianza kuzagaa kwa kasi juzi saa 2:00 usiku na kusababisha taharuki katika Miji ya Moshi na Arusha.
No comments:
Post a Comment