Tuesday, 13 August 2013

DOGO JANJA AMPIGIA MAGOTI MADEE ILI AMRUDISHE TENA TIP TOP CONNECTION Kuna kila ishara kuwa meli ya Watanashati Entertainment iliyomchukua Dogo Janja kwa mbwembwe nyingi, inaelekea kuzama na abiria wawili waliosalia, Dogo Janjaro na PNC wameanza kutafuta maboya haraka kujihami.

Kwa mujibu wa meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale, Dogo Janja amekuwa akimpigia simu Madee ili wakae chini waongee kumaliza tofauti zao na ili arejee Tip Top.
“Unavyomwona Dogo Janja leo hii anampigia simu Madee kumwomba wakae chini,” alisema Tale kwenye kipindi cha Mkasi.
 
“Ni kwamba wale marafiki hawapo tena. Leo hii kwakuwa Dogo Janja anamhitaji Madee atausema ukweli. Dogo Janja hela yake alikuwa anampa mshkaji mmoja anaitwa Doka. Mimi niliyajua hayo baada ya matatizo.”
Dogo Janja alijiondoa Tip Top June mwaka jana kwa madai kibao ikiwa pamoja na kudai kwamba hakuwahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.
 
Alidai kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.
 
“Nilikuwa navumilia tu, kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” alikaririwa kwenye kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.