Wednesday 14 August 2013

FERA APIGWA MPAKA KUTOA MAVI HUKO SUMBAWANGA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIPENDELEA TIMU YA MUCHIZA FC


Mwamuzi na wachezaji watatu wa timu ya Serengeti SC ya wilayani Sumbawanga mkoani  Rukwa wamelazwa kwenye kituo cha Afya cha Laela baada kushambuliwa na kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili katika mchezo wa Ligi ya ujirani mwema.

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kisalala kata ya Laela, ulitamatia dakika ya 75 baada ya kundi la mashabiki wa Serengeti FC kuanza kumshambulia mwamuzi kwa kumvua nguo na kisha  kumpiga mwamuzi Eliaza Simsokwe na hadi akajisaidia haja kubwa( kunya  mavituzi).


 Inadaiwa sababu ya kumpiga mwamuzi huyo ni kupinga bao lililofungwa na mchezaji wa timu pinzani ya Muchiza FC, Siyaye Mgonde wakidai alikuwa ameotea kabla ya kufunga.




Mwanamke mmoja alimsaidia mwamuzi huyo kwa kumfunga khanga ili kumsitiri baada ya kuvuliwa nguo.

Wachezaji wawili na kocha watimu ya Serengeti walijeruhiwa na kulazwa kwenye kituo hicho cha Afya.

Aidha ugomvi huo uliibuka tena majira ya usiku nje ya uwanja ambako watu wanaodaiwa kuwa ni wakazi wa kijiji cha Kisalala walivamia tena wachezaji wa timu ya Serengeti FC na kumjeruhi Peter Willy  ambaye   alijeruhiwa kwa kupigwa panga kichwani na kusababishiwa jeraha kubwa.

Uongozi wa Chama cha soka wilayani Sumbawanga (SURUFA) kupitia kwa katibu wake, Kanyiki Nsokolo umesema kufanyika kwa vitendo hivyo ni matokeo ya kuendesha masuala ya soka kienyeji pasipo kufuata taratibu ikiwa ni pamoja mashindano hayo kufanywa pasipo kukishirikisha chama cha soka cha wilaya sanjari na kutokuwapo kwa makocha  na waamuzi wenye sifa kwa ajili ya kuchezesha michezo mbalimbali ya soka.

No comments:

Post a Comment