Monday 12 August 2013

"NIKIFA SIHITAJI KAMATI YOYOTE YA KUENDESHA MSIBA WANGU .....KAMA WALIKULA ZA NGWEA, WATASHINDWA NINI KWANGU?".. NAY WA MITEGO



 MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego, ameweka wazi kuwa ikitokea amefariki dunia hatohitaji kamati kwa ajili ya kuendesha mipango ya msiba wake, kwa kile anachodai kuwa kamati hizo zipo kwa ajili ya kuvuna pesa.

Hayo aliweka wazi baada kupokea ujumbe mfupi kwenye simu yake wenye vitisho uliotokana na mashairi alioimba kwenye single yake mpya ya 'Salaam zao' .

Ujumbe huo wa vitisho ambao umepokelewa na msanii huyo umekuja mara baada ya msanii huyo kuachia single yake hiyo ambapo moja ya mashahiri ni juu ya hela za rambirambi zilizopatikana katika msiba wa msanii Ngwear pamoja na Kanumba kushindwa kuwafikia walengwa.

Akizungumza na jarida la Maisha, mara baada ya kutuma ujumbe alioupokea wa vitisho kwenye ukurasa wake wa 'Instagram', Ney wa Mitego aliweka wazi kuwa amepokea ujumbe wa vitisho mara baada ya kuachia nyimbo hiyo.

Alisema kuwa amepokea ujumbe mbalimbali ambazo zipo zinazowataja wahusika moja kwa moja wale waliohusika kula rambirambi, huku wengine wakimtumia ujumbe wa kumtisha kwa kile alichokiimba katika nyimbo hiyo.

"Mimi hata ikitokea nakufa leo sihitaji mtu yeyote wa  kuweka  kamati ya mazishi yangu kwani najua kitakachotokea siyo mazishi bali ni kula hela na rambirambi hizo kushindwa kutimiza malengo kama yalivyokusudiwa" alisema Ney wa Mitego.

Aliongezea kuwa hawezi kuacha kuimba ukweli hata kama ataendelea kupokea vitisho.

No comments:

Post a Comment